Matukio ya siku ya 7 tangu kuanza mapigano kati ya Israel na Palestina
Zaidi ya watu milioni moja wamelazimika kukimbia kutoka makazi yao kaskazini mwa ukanda wa Gaza mwishoni mwa wiki hii tangu Israel kuanza mashambulio dhidi ya kundi la Hamas, huku Umoja wa Mataifa ukionya hali ni mbaya kabisa katikia ukanda huo.

1
Wafuasi wa chama cha kisiasa na kidini cha Pakistan cha Jamaat-e-Islami wahudhuria maandamano dhidi ya mashambulio ya anga ya Israel huko Gaza, na kuwaunga mkono wa Palestina mjini Karachi, Pakistan. Jumapili Oct 15, 2023.

2
Waandamanaji wakibeba mabango yenye maandishi yanayounga mkono watu wa Palestina katika mji mkuu wa Hispania wa Madrid. Oktoba 15, 2023.

3
Watu waandamana kuunga mkono watu wa Israel katika ufukwe wa Copacabana mjini Rio de Janeiro, Brazil Oktoba 15, 2023.

4
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Antony Blinken azungumza na waandishi habari mjini Cairo kabla ya kuelekea Jordan, akiwa kwenye ziara ndefu ya nchi za Mashariki ya Kati kutafuta njia za kuzuia mapigano ya Gaza, kati ya Israel na Hamas.
Forum