Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 12:06

Uamuzi wa mahakama ya Juu Marekani kupinga sera ya kusajili wanafunzi wa vyuo vikuu waibua utata


Supreme Court Affirmative Action
Supreme Court Affirmative Action

Mahakama ya Juu ya Marekani Alhamisi imeamuru kwamba sera inayotoa nafasi mbalimbali kwa watu waliotengwa, maarufu kama Affirmative Action, kujiunga na vyuo vikuu nchini Mrekani, kwa kuzingatia rangi ya mtu, unakiuka katiba.

Katika uamuzi wa majaji 6 dhidi ya watatu, mpango huo sasa umebatislishwa, kwenye Chuo Kikuu cha Harvard, na Chuo Kikuu cha North Carolina.

Uamuzi huo wa kihistoria una umuhimu mkubwa kitaifa, na umepokelewa kwa hisia mseto na Wamarekani wa tabaka mbalimbali, wakiwemo wanafunzi na wanasiasa wa mirengo yote.

Jaji Mkuu John Roberts alisema kwamba kwa muda mrefu sana, vyuo vikuu "vimehitimisha, kimakosa, kwamba msingi wa utambulisho wa mtu binafsi si changamoto zinazotolewa, ujuzi unaojengwa, au mafunzo wanayojifunza bali ni rangi ya ngozi yao. Historia ya katiba yetu haivumilii hali hiyo."

Uamuzi huo utalazimisha vyuo na vyuo vikuu kote Marekani kutafuta njia mpya za kufikia uandikishaji wa wanafunzi mbalimbali bila kuzingatia rangi, kama vile kuangalia kwa karibu zaidi hali ya kiuchumi ya familia za wanafunzi wanaotarajiwa na asili ya jamii walikokulia.

Punde tu baada ya uamuzi huo kutolewa, waandamanaji walikusanyika nje ya mahakama ya juu mjini Washington DC, wengi wakipinga yaliyojiri.

Rais Joe Biden alizungumzia suala hilo kwati ikulu na kusema kwamba "uamuzi huo haukubaliki."

"Hatuwezi kukubali uamuzi huu uwe ndio wa mwisho kuhusu suala hili," alisema.

Ubaguzi unalipo nchini Marekani. Tunahitaji mfumo wa elimu ya juu ambao umnamfaidi kila mtu," aliongeza.

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, ambaye anawania tikiti ya chama chake caha Republican, ili kugombea urais kwa mara nyingine mwaka ujao, alisifu uamuzi huo na kusema kwamba unatoa haki kwa usawa kwa Wamarekani.

Forum

XS
SM
MD
LG