Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 22:53

Hakuna makubaliano mapya ya nyuklia kati ya Marekani na Iran, asema Blinken


Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken Jumatano amesema kwamba hakuna makubaliano mapya ya nyuklia na Iran yanayeondelea kujadiliawa, licha ya hatua kadhaa za kidiplomasia zilizopigwa kati ya Marekani na taifa hilo hasimu katika siku za karibuni.

Blinken wakati akizungumza mbele ya baraza la Uhusiano wa Kigeni la Umoja wa Mataifa mjini New York, amesema kwamba, “ Hakuna makubaliano yaliojadiliwa, licha ya kuwa tuna nia ya kuendelea kuzingatia njia za kidiplomasia.” “Tunatazama mwenendo wao,” ameongeza Blinken , akiomba Iran kujiepusha na njia zinazoweza kuongeza taharuki kati yake na Marekani pamoja na mataifa ya mashariki ya kati.

Rais wa Marekani Joe Biden alichukua madaraka kwa matumaini ya kurejesha mkataba wa nyuklia wa 2015 na Iran, baada ya kusitishwa na mtangulizi wake Donald Trump. Hata hivyo mazungumzo yaliokuwa yakiongozwa na EU yalivunjika, huku kukizuka maandamano makali nchini humo, hali iliyopelekea Marekani kusita kuingia kwenye mkataba mpya na taifa hilo lenye misimamo mikali ya kidini.

Forum

XS
SM
MD
LG