Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 20:42

Paris: Mikutano inayotarajiwa kuhusisha upigaji kura kuikubali Marekani kurejea UNESCO yaanza


Rais wa Marekani Joe Biden

Wanachama wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Utamaduni  wanakutana Alhamisi kuanza mikutano ya siku mbili mjini  Paris inayotarajiwa kuhusisha upigaji kura kuikubali Marekani kurejea katika shirika hilo.

Marekani ilijiondoa mwaka 2018 ikilalamika kuhusu msimamo dhidi ya Israeli na utawala mbaya katika shirika hilo.

Kabla ya kujiondoa, Marekani ilikuwa ni mfadhili pekee mkubwa zaidi wa UNESCO, ikitoa takriban moja ya tano ya ufadhili wote kwa shirika hilo.

Maafisa wa Marekani walisema mapema mwezi huu kuwa shauku yao ya kurejea UNESCO ilichochewa na wasiwasi kuhusu ushawishi wa China katika uwekaji wa sera kwenye shirika hilo, hususan zile za akili bandia (artificial intelligence) na mafunzo ya teknolojia.

Kama sehemu ya pendekezo la mpango wa kurejea katika shirika hilo, utawala wa Biden umeomba dola za Kimarekani milioni 150 kwa ajili ya ufadhili wa michango na madeni yake kwa UNESCO.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii zinatokana na mashirika ya habari ya AP na Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG