Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 06, 2024 Local time: 11:27

Marekani kujiunga tena na UNESCO


Nembo ya UNESCO yaonekana wakati wa ufunguzi wa kongamano la 39 la shirika hilo kwenye makao yake makuu mjini Paris.
Nembo ya UNESCO yaonekana wakati wa ufunguzi wa kongamano la 39 la shirika hilo kwenye makao yake makuu mjini Paris.

Marekani inapanga kujiunga tena na shirika la Umoja wa mataifa la Sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) kuanzia mwezi ujao wa Julai, UNESCO imesema Jumatatu.

Marekani ilijindoa kwenye shirika hilo mwezi Disemba mwaka wa 2018 chini ya utawala wa Rais Donald Trump kwa madai kuwa UNESCO inachukua hatua za kuegemea dhidi ya Israel na usimamizi wake ni mbaya.

“Ni kitendo cha imani ya dhati kwa UNESCO na ushirikiano wa kimataifa,” mkurugenzi mkuu wa UNESCO Audrey Azoulay amesema katika taarifa akitangaza Marekani kujiunga tena na shirika hilo.

Mpango uliopendekezwa lazima uwasilishwe kwa kongamano kuu la nchi wanachama wa UNESCO ili kuidhinishwa, na baadhi ya nchi wanachama zimeitisha kikao maalum kitakachofanyika siku za usoni ili kuchukua maamuzi.

Marekani inachangia asilimia 25 ya fedha kwenye shirika hilo lenya makao yake mjini Paris.

Forum

XS
SM
MD
LG