Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 14, 2024 Local time: 09:31

11 wauawa katika shambulizi la kulipiza kisasi la Marekani nchini Syria


Ndege za kivita za Marekani
Ndege za kivita za Marekani

Wapiganaji 11 wanaoiunga mkono Iran waliuawa katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani dhidi ya Syria, ambayo ni ya kulipiza kisasi, kufuatia shambulio la ndege isiyo na rubani, lililosababisha kifo cha Mmarekani mmoja na kuwajeruhi wengine sita.

Mkandarasi wa Marekani aliuawa, na mkandarasi mwingine na wafanyakazi watano wa Marekani kujeruhiwa, wakati ndege isiyo na rubani ya kamikaze ambayo inaelezwa kuwa "yenye asili ya Iran" ilipogonga kituo cha matengenezo kwenye kambi ya muungano wa kijeshi unaoongozwa na Marekani karibu na Hasakeh, kaskazini mashariki mwa Syria, Pentagon ilisema.

Katika kujibu, Waziri wa Ulinzi wa Marekani Lloyd Austin alisema kwamba, kwa maelekezo ya Rais Joe Biden, aliamuru "mashambulizi ya anga huko mashariki mwa Syria, dhidi ya vituo vinavyotumiwa na makundi yenye uhusiano na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran".

"Mashambulio hayo ya anga yalifanywa kujibu mashambulizi ya leo pamoja na mfululizo wa mashambulizi ya hivi majuzi dhidi ya vikosi vya muungano nchini Syria na makundi yenye uhusiano na IRGC," Austin alisema.

Shirika la Uangalizi wa Haki za Binadamu la Syria, mfuatiliaji mwenye makao yake makuu nchini Uingereza na mtandao mpana wa vyanzo vya habari katika nchi hiyo yenye vita, limesema watu 11 wameuawa kutokana na mashambulizi ya Marekani, wakiwemo Wasyria wawili.

Marekani imetuma takriban wanajeshi 900 katika kambi na vituo kaskazini mashariki mwa Syria kama sehemu ya muungano wa kimataifa unaopambana na wapiganaji waliosalia, wa kundi la Islamic State (IS).

XS
SM
MD
LG