Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 19:43

Rais wa Syria atembelea UAE


Rais wa Syria, Bashar al Assad, amewasili katika Umoja wa  Falme za Kiarabu Jumapili kwa ziara rasmi akiwa pamoja na mke wake Asma al Assad, katika kipindi ambacho mataifa ya kiarabu yameonyesha kulegeza kuitenga Damascus.

Ziara hiyo inaonekana sherehe zaidi ikilinganishwa na ziara ya nyuma alipokwenda Emarati mwaka jana ambayo ilikuwa ya kwanza katika taifa la kiarabu toka kuanza vita vya wenyewe kwa wenyewe mwaka 2011.

Katika kipindi hicho mataifa ya Ghuba ikijumuisha UAE yaliwaunga mkono waasi ili kumuondoa Assad madarakani.

Chombo cha habari cha serekali kimeripoti kwamba alikutana na rais Sheikh Mohammed bin Zayed al-Nahyan alipowasili Abu Dhabi, Jumapili, na kupewa heshima ya saluti wakati ujumbe wake ulipokuwa ukiingia kwenye makazi ya kifalme. Ndege ya Assad ilipokelewa na ndege za kivita za Emarati

XS
SM
MD
LG