Takriban watu 30 waliokolewa na mmoja kupelekwa hospitalini, kikosi cha zima moto kilisema kwenye taarifa iliyochapishwa kwenye mitandao ya kijamii.
Waokoaji walisema walitumwa kwa maeneo kadhaa yaliyofurika tangu saa tisa asubuhi, na kuongeza kwamba juhudi zao za uokoaji bado zinaendelea.
Mvua kubwa ilinyesha usiku kucha, ina kusabisha vitongoji vingi vya Abidjan kufurika, na kuzifanya barabara kuu kadhaa, zisitumike.
Wakazi walichapisha picha kwenye mitandao ya kijamii zinazoonyesha ukubwa wa mafuriko hayo katika nyumba zao, au kwenye vitongoji wanamoishi, na kuomba msaada.
Wiki iliyopita, watu sita walikufa baada ya mvua kubwa kusababisha maporomoko ya ardhi katika kitongoji cha magharibi mwa mji wa Mossikro.
Maporomoko ya ardhi wakati wa msimu wa mvua ni jambo la kawaida katika mji wa Abidjan, ambao unakua kwa kasi na ulio na wakazi takriban milioni tano.
Mafuriko ya awali yalisababisha vifo vya watu 18 hapo mwezi Juni mwaka wa 2018 na 13, mnamo mwezi Juni 2020.