Idadi ya vifo kutokana na mafuriko huko Ghana imeongezeka na kufikia 30 kutoka watu 23 Jumatatu. Kofi portuphy, mratibu wa idara inayohusika na majanga huko Ghana, alithibitisha idadi mpya ya vifo kwa waandishi wa habar Jumanne. Mafuriko mengi yametokea katika maeneo ya karibu na mji mkuu, Accra na kati kati ya Ghana. Mafuriko yaliyosababishwa na mvua kali, yamebeba magari, yameharibu nyumba na kuwakosesha makazi mamia ya watu. Maafisa wa Ghana wanasema mafuriko haya ni mabaya kuliko yote kupata kutokea katika historia ya hivi karibuni. Kipindi cha mvua cha mwaka Afrika Magharibi siku zote husababisha mafuriko makubwa . Mwaka 2009 mafuriko yaliuwa zaidi ya watu 100 na wengine zaidi ya milioni 2.5 kupoteza makazi yao katika nchi 8.
30 wafariki kwenye mafuriko Ghana

Idadi ya vifo kutokana na mafuriko huko Ghana imeongezeka na kufikia 30 kutoka watu 23 Jumatatu.