Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 17:35

Mafuriko yazusha shida Dar Es Salaam


Mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar Es Salaam zimeathiri makazi ya watu na miundo mbinu
Mvua kubwa zinazonyesha jijini Dar Es Salaam zimeathiri makazi ya watu na miundo mbinu

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar Es Salaam zaleta athari kwenye makazi ya watu na miundombinu katika eneo

Jiji la Dar Es Salaam, Tanzania limekumbwa na mafuriko makubwa ambayo wakazi wa miaka mingi mjini humo wanasema hayajapata kutokea katika mji huo. Mvua zilizoanza kunyesha Jumanne alfajiri zimeendelea tena Jumatano asubuhi jijini humo na kuchochea kuongezeka kwa mafuriko katika maeneo kadhaa ya jiji hilo, pamoja na athari kubwa kwenye miundombinu na makazi ya watu, ambapo inasadikiwa watu wapatao wanane wamepoteza maisha.

Hata hivyo idadi ya vifo hivyo huenda ni kubwa zaidi ya ilivyotolewa na uongozi wa mkoa wa Dar es salaam kutokana na wasi wasi kwamba watu wengi bado hawajaokolewa wakibaki wamezingirwa na maji na kufanya jitihada binafsi za kujiokoa.

Wakazi wapatao zaidi ya 600 hawana mahali pa kuishi kutokana na nyumba zao kujaa maji na nyingine kubomolewa kabisa. Baadhi ya nyumba katika maeneo ya mabondeni zimezama kwa zaidi ya asilimia tisini huku nyingine zikiwa zimeanguka kabisa kutokana na mafuriko hayo.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadick amesema hivi sasa juhudi zinafanywa kuendelea kuokoa watu waliozingirwa na maji kwa kuwadondoshea makoti maalum ya kuogelea kwa njia ya helikopta huku serikali pia ikitenga maeneo maalum kwa ajili ya watu walioathirika na mafuriko hayo jijini dar es salaam .

Miundo mbinu hafifu imetajwa kuwa chanzo kikubwa cha mafuriko katika jiji la dar es salaam na maeneo mengine nchini ambayo nayo kwa sasa yamekumbwa na mafuriko makubw aikiwemo mikoa ya mwanza na mbeya.

James Mbatia mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI ameituhumu serikali kwanza kwa kutokuwa wepesi kukabili majanga kama hayo na pia kuwa chanzo cha majanga haya kutokana na kutokwua na mipango sahihi ya miji na miundombinu mibovu.

Wito wa serikali ya mkoa wa Dar es salaam kwa wakazi wa jiji hili ni kwa wanaoishi mabondeni kuhama haraka kwa kuwa kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa hali hii ya mvua kubwa inatarajiwa kuendelea. jioni hii vikosi vya jeshi la majini lilianza kufanya kazi ya kuokoa watu pamoja na maiti zinazodhaniwa bado kuwepo kweney maeneo ya mafuriko.

XS
SM
MD
LG