Taasisi ya Waislamu wa Amerika ya Ksakazini ICNA imeanda kongamano lake la kila mwaka mjini Baltimore, Maryland, kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitatu ya janga la COVID, Mkusanyiko huo ambao ndio mkubwa kabisa wa waislamu hapa marekani unahudhuriwa na zaidi ya wajumbe elfu 20 kulingana na watayarishaji wake. Kongamano hilo linawaleta pamoja wasomi wafanaya bishara waatalamu wa masuala mbali mabli pamoja na vijana, kujadili masuala yanaohusiana na maisha ya waislamu na changamoto zilizopo.
Kongamano la Waislamu wa Marekani na Canada ICNA lafunguliwa Baltimore
Zaidi ya watu elfu 22 wahudhuria kongamano kubwa kabisa la waslamu wa Marekani na Canada, linalofanyika kila mwaka na kusimamiwa na taasisi ya ICNA

1
Kikao cha ufunguzi waKongamano la waislamu Icna Marekani mjini Baltimore, Maryland, Mei 28, 2022

2
wajumbe wakielekea kwenye vikao mbali mbali wakati wa kongamano la ICNA mjini Baltimore, Maryland

3
Kibanda cha Shirika la UMR, linalotetea haki za watoto na kuwasidia watoto wanaoteswa na kufanyishwa kazi.

4
Kibanda cha kuuza maandishi ya kidini yaliyochongwa kwenye mbao kwenye kongasmano la ICNA