Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 12:31

Ujumbe wa Marekani wafanya mazungumzo na ujumbe wa Maduro


Nicolas Maduro, kiongozi wa Venezuela
Nicolas Maduro, kiongozi wa Venezuela

Ujumbe wa maafisa waandamizi wa Marekani ulikwenda nchini Venezuela Jumamosi kwa mazungumzo na wajumbe wa serikali ya Rais Nicolas Maduro kuangalia uwezekano wa kupunguza vikwazo vya Marekani dhidi ya taifa hilo ambalo ni mzalishaji mkubwa sana wa mafuta kwa mujibu wa vyanzo ambavyo vilishiriki katika mazungumzo hayo.

Vyanzo vinasema mazungumzo yamekuwa yakifanyika kwa siri kwa miezi kadhaa huku utawala wa Biden ukipima njia ya kupunguza vikwazo na kushauriana kuhusu kuachiliwa kwa raia wa Marekani ambao wameshikiliwa nchini Venezuela. Lakini wanasema mazungumzo yalichukua mwelekeo wa haraka kutokana na uvamizi wa Russia nchini Ukraine.

Marekani chini ya utawala wa Rais wa zamani Donald Trump ulifunga mahusiano ya kidiploamsia na Venezuela mwaka 2019 baada ya Marekani kumtambua kiongozi wa upinzani Juan Guaido kama rais halali wa nchi hiyo na kumshutumu Maduro kwa wizi wa kura katika uchaguzi ambao alichaguliwa tena. Utawala wa Trump pia ulizuia mapato yote ya Marekani kwa kampuni ya taifa ya mafuta ya Venezuela.

Jarida la Wall Street linaripoti kwamba katika wiki za karibuni baadhi ya wawekezaji wa Marekani wameutaka utawala wa Biden kuondoa vikwazo kwa Venezuela ili iweze kupeleka mafuta ghafi zaidi katika soko. Hiyo itaondoa mwanya kama mataifa ya Magharibi yataamua kususia mafuta ya Russia.

White House, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, na Wizara ya Habari ya Venezuela wamekataa kutoa maoni ya moja kwa moja kuhusu mazungumzo hayo.

XS
SM
MD
LG