Meja Jenerali Abel Kandiho aitakiwa kuondoka kwenye wadhifa wake kama mjumbe wa usalama nchini Sudan Kusini, wiki mbili tu baada ya kuachishwa kazi kama mkuu wa ujasusi.
Msemaji wa jeshi la Uganda Luteni Kanali Ronald Kakurungu amesema katika taarifa “Kandiho ameteuliwa kwenye nafasi ya mkuu wa jeshi la polisi la Uganda”.
Kufikia mwezi uliopita, Kandiho alikuwa kamanda wa idara ya upelelezi katika jeshi na alikabiliwa na tuhuma kadhaa za unyanyasaji, ikiwa ni pamoja na kuwapiga watu, dhulma ya kingono na kuwapiga watu na vifaa vya umeme.
Wizara ya fedha ya Marekani ilimwekea vikwazo Kandiho mwezi Disemba mwaka jana, kwa madai ya ukiukaji wa haki za binadamu uliofanyika chini ya uongozi wake kama mkuu wa upelelezi katika jeshi la Uganda.