Mpaka huo ulifungwa mwaka 2019 kufuatia mivutano baina ya mataifa hayo ya Afrika mashariki.
Kwa upande wa Uganda, ujenzi wa ofisi za forodha ambazo ni sehemu ya mfumo wa kituo kimoja cha mpakani unaotekelezwa katika jumuiya ya Afrika mashariki unaendelea.
Tangazo la kufunguliwa tena mpaka lilitolewa wiki iliyopita baada ya mkutano baina ya rais wa Rwanda Paul Kagame na Luteni Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa kiume wa rais Yoweri Museveni.
Rwanda iliishutumu Uganda kwa kuwashikilia na kutesa raia wake wakati Uganda nayo iliishutumu Rwanda kuingilia ujasusi wake wa kijeshi. Nchi zote zimekanusha shutuma hizo.
Facebook Forum