Makamanda hao wamekutana kufanya uchunguzi na ukaguzi wa kazi walizozifanya pamoja tangu Novemba mwaka 2021 hadi sasa huku lengo likiwa ni kuwasaka waasi wa ADF katika misitu ya Beni.
Operesheni hiyo inafanywa chini ya uongozi wa Luteni Jenarali Muhanga Kayanja kwa upande wa Jeshi la Uganda na Upande wa FARDC ukiongozwa na meja Jenerali Kamile Bombele.
Maofisa hao wamepongeza hatua na kazi ambazo zimefanyika na bado zinaendelea. Katika kikao chao wametangaza mafanikio makubwa dhidi ya waasi wa ADF .
Kuhusu mkutano huo wa kijeshi Austere Malivika alizungumuza na Mbunge wa Chama tawala, UDPS, Shabola Bintou akiwa kwenye ziara eneo la mashariki kufanya uchunguzi kuhusu kazi za usalama.
Mbunge huyo wa chama tawala cha UDPS anasema: "Makamanda hao wameamua kuendelea na operesheni za kijeshi hadi katika Mkoa jirani wa Ituri kama njia moja ya kutokomeza mauaji ya mara kwa mara yanayotekelezwa na makundi ya waasi kama Vile ya CODECO .