Wakati huohuo wafuasi wa kiongozi wa wanamgambo wa Libya Khalifa Haftar walishiriki katika mkusanyiko wa umma upende wa mashariki wa bandari ya mji wa Benghazi, Libya Julai 5, 2020, wakipinga hatua ya Uturuki kuingilia kati masuala ya Libya.
Wabunge wa Misri wakutana Cairo kujadili hatma ya kupeleka vikosi Libya
Bunge la Misri katika kikao chake cha ndani Julai 20, ilipitisha uwezekano wa kupeleka vikosi nchini Libya kumuunga mkono Khalifa Haftar ambaye ni rafiki wa Cairo, iwapo vikosi vinavyosaidiwa na Uturuki vitauteka tena mji wa Sirte.
5
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu, kulia, na Waziri wa Ulinzi wa Uturuki Hulusi Akar wakishiriki katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergey Lavrov na Waziri wa Ulinzi wa Russia Sergei Shoigu mjini Moscow, Russia, Jumatatu, Jan. 13, 2020. Hii ni juhudi ya panda zote mbili kudhamini mkutano utakao washirikisha pande hasimu zinazopigana nchini Libya kushiriki katika mazungumzo hayo Moscow.. (AP Photo/Pavel Golovkin, Pool)