Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 18:55

Tundu Lissu wa Chadema apigwa risasi nchini Tanzania


Tundu Lissu
Tundu Lissu

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu, amejeruhiwa kwa risasi.

Vyanzo vya habari nchini Tanzania vinasema kuwa ameshambuliwa kwa risasi wakati akishuka nyumbani kwake Area D Mjini Dodoma, alikuwa akitokea Bungeni na alienda Nyumbani kula chakula cha mchana.

Inadaiwa kuwa Lissu amepigwa risasi 5, miguuni na tumboni. Kwa sasa wapo hospitali ya Mkoa, mjini Dodoma.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hali ya Mbunge huyo aliye hospitalini sasa ni mbaya.

XS
SM
MD
LG