Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 23:12

Watu wanne wauawa kwa kukatwa vichwa Kenya


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Watu wanne wameuawa kwa kukatwa vichwa vyao katika eneo la Hindi kaunti ya Lamu, Kenya usiku wa kuamkia Jumatano.

Kulingana na wanakijiji watu waliokuwa wamevalia magwanda ya polisi walivamia vijiji viwili vya Bobo na Silini ambako inadaiwa waliwaita kwa majina watu hao kabla ya kuwatendea nyama huo.

Kamanda wa polisi kaunti ya Lamu Gilbert Kitiyo amethibitisha tukio hilo huku akisema kuwa wanaendelea na uchunguzi kubainisha ikiwa mauaji hayo yalitekelezwa na Al Shabaab au wahalifu katika eneo hilo.

Duru zinadokeza kuwa huenda mauaji hayo yametokana na mzozo kati ya jamii ya wafugaji na wakulima ambao huzozania sehemu za kuendeleza shughuli zao.

Wakaazi katika maeneo ya Hindi na Lamu wamefanya maandamano wakilalamikia utepetevu wa maafisa wa polisi ambao walikosa kufika kwa haraka hata baada ya wanakijiji kupiga kamsa.

Usafiri wa mabasi kutoka eneo la Mpeketoni Lamu kuelekea Mombasa imetatizika kwa ajili ya maandamano huku hali ya usalama katika barabara hiyo ikiwa bado ni hatari kutokana na vilipuzi vya kuwekwa ardhini.

Hali hiyo imetatiza usafiri wa mabasi na hata magari ya kibinafsi ambapo maafisa wa kijeshi ni lazima kuyasindikiza magari hayo.

XS
SM
MD
LG