Karibu wakimbizi 7000 walokimbia mauwaji yanayofanywa na wanamgambo wa kislamu wa kundi la Boko Haram huko Nigeria na Niger wanaishi katika kambi ya Dar Es Salam katika mji wa Baga-Sola, magharibi ya Chad.
Wakimbizi wa Kinigeria katika kambi ya Dar Es Salam, Magharibi ya Chad
1
Mamia ya watoto ni miongoni mwa wakimbizi takriban 7000 wanaoishi kwenye kambi ya Dar Es Salam huko Baga-Sola Chad April 2 2016.
2
Wakimbizi wanaishi katika jangwa kukiwa na joto kali kwenye kambi ya Dar Es Salam huko Baga-Sola Chad.
3
Wakimbizi ndani ya hema ambayo ni makazi yao kwenye kambi ya Dar Es Salam huko Baga-Sola magharibi ya Chad.
4
Mwanamke huyu mkimbizi ana wasi wasi hajapata habari za mumewe kutoka Nigeria tangu akimbiye mwaka mmoja uliyopita na kuwasili huko, Baga-Sola, Chad.