Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:33

Upinzani wataka mawaziri walioteuliwa kufanya kazi kwa bidii


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mkutano na baraza lake la mawaziri alipokutana na rais Obama.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mkutano na baraza lake la mawaziri alipokutana na rais Obama.

Baada ya rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kufanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri siku ya Jumanne, wakenya wengi wameendelea kutoa hisia zao mbali mbali.

Bw.Kenyatta aliwatimua mawaziri 6 wanaotuhumiwa kwa rushwa na wizi wa fedha za serikali na vile vile akapanua baraza lake la mawaziri na kuongeza idadi ya wizara za serikali.

please wait

No media source currently available

0:00 0:06:26 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mbunge wa upinzani nchini Kenya, Richard Onyonka, alizungumza na Sauti ya Amerika na kueleza kwamba anaamini kutakuwa na mabadiliko kwa sababu rais alifanya vizuri kuwaondoa wale waliotuhumiwa.

"Mimi nina uhakika kuwa wale mawaziri amewataja sasa wako safi hawana shida ya ufisadi wakati huu lakini unajua vile mnavyosema, hata umesema wewe mwenyewe ufisadi ni kama ugonjwa, lazima wale ambao rais amewateuwa wajue kuwa macho ya wakenya yanawaangalia." alisema Bw.Onyoka.

XS
SM
MD
LG