Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 02, 2024 Local time: 23:16

Wakazi wa Morocco wasema tetemeko kubwa lililopiga limeonyesha ustahmilivu na ari ya watu


Msichana akipokea mikate kutoka kwa watu wanaojitolea huku wengine wakiwa wanangojea katika magari kifusi kiondolewe njiani kufuatia janga lililosababisha vifo la tetemeko la ardhi karibu na kijiji cha Tallat n'Yakoub, Morocco, Sept. 12, 2023
Msichana akipokea mikate kutoka kwa watu wanaojitolea huku wengine wakiwa wanangojea katika magari kifusi kiondolewe njiani kufuatia janga lililosababisha vifo la tetemeko la ardhi karibu na kijiji cha Tallat n'Yakoub, Morocco, Sept. 12, 2023

Uharibifu uliosababishwa na tetemeko kubwa la ardhi kupiga nchini Morocco katika kipindi cha zaidi ya karne moja limekuwa na athari kubwa. Lakini wakazi wanasema pia limeonyesha ustahmilivu na ari ya watu.

Mji wa Moulay Brahim uko karibu na kiini cha tetemeko la ardhi ambalo lilipiga Morocco Septemba 8. Hii inaelezea siyo tu kiwango cha uharibifu uliorekodiwa hapo, lakini pia mmiminiko wa watu kutoka katika vijiji vingine na miji ambao walifika kusaidia juhudi za uokoaji.

Yacine Alfassal kutoka Marrakech, anasema watu wengi hawana walichobakiwa nacho – hawana chakula, hawana pa kulala, hawana chochote.

“Nimeona watu wangapi wamebaki hawana chochote – hawana chakula, hawana pa kulala, hawana cha kuwaendeshea masiha – hakuna hata mmoja aliyebaki tofauti. Kwa nawapenda watu wote kama mimi ambao tunaishi Marrakesh, kwasababu nafahamu huko kuna mambo mengi. Napenda sisi tuwaangalie watu wachache, siyo tu hivi sasa: ningependa kuwaangalia hivi sasa na kuwasiliana nao, na kati siku za usoni kuwa na mawasiliano nao,” anasema Yacine.

Kaburi linachimbwa kuwazika waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katika kijiji cha Ouargane, karibu na Marrakech, Morocco, Sept. 9, 2023.
Kaburi linachimbwa kuwazika waliofariki kutokana na tetemeko la ardhi katika kijiji cha Ouargane, karibu na Marrakech, Morocco, Sept. 9, 2023.

Baada ya kusadia kuwazika jamaa 22, mkazi wa Moulay Brahim Abdelhamid Aouzal alijiunga katika juhudi za kukusanya misaada kwa wale wenye shida. “Tunajaribu kuweka pamoja kila kitu ambacho tumepokea kutoka kwa raia na wakazi wa vijiji vingine. Tunajaribu kukusanya kila kitu hapa katika makao makuu ya shirika hili. Tumeandaa mipango ya ugawaji baadaye. Kuna familia katika maeneo kadhaa yanayozunguka hapa, ambayo bado yako kazini.”

Badder Manaouch, mwalimu wa shule ya msingi ambaye anawafundisha watoto katika eneo la milimani la High Atlas nchini Morocco kwenye kijiji karibu na mji wa Asilah anakubaliana na maelezo ya wale walioko huko kuhusu jinsi raia walivyokuja pamoja katika janga hili.

“Hawana chochote, lakini wanatoa. Hili linajulikana vizuri kuhusu wtu wa Morocco. Watu wa Morocco wako tayari na halafu utawaona wako huko kila inapokuwa ni suala la ushirikiano au mshikamano. Kil awakati kuna mtu sehemu fulani nchini Morocco anahitaji kitu fulani, na wanakipata,” anasema Badder.

Tetemeko kubwa la ardhi limepiga milima ya High Atlas, na kuua takriban watu elfu tatu na kujeruhi wengine zaidi ya 5,000, kwa mujibu wa hesabu rasmi. Tetemeko la ardhi nchini humo ni bay asana tangu mwaka 1960.

Forum

XS
SM
MD
LG