Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 17, 2024 Local time: 12:13

Manusura wa tetemeko la ardhi Morocco wajaribu kuishi katika makazi ya muda katika siku ya nne


Mmoja wa wazee katika kijiji akiangalia kijiji chake cha Douzrou kilivyoharibiwa na tetemeko la ardhi huko jimbo la al-Haouz katika Milima ya High Atlas katikati ya Morocco on Septemba 12, 2023.
Mmoja wa wazee katika kijiji akiangalia kijiji chake cha Douzrou kilivyoharibiwa na tetemeko la ardhi huko jimbo la al-Haouz katika Milima ya High Atlas katikati ya Morocco on Septemba 12, 2023.

Manusura wa tetemeko la ardhi lililosababisha vifo katika mji wa Talat N’Yaaqoub walikuwa wakijaribu kuishi katika makazi ya muda Jumanne (Septemba 13) baada ya kuwa wanaishi nje katika siku ya nne.

Usiku kucha, wale waliokuwa hawana mahema walilala ndani ya mablanketi chini, wakipika katika eneo la wazi kutokana na chakula cha msaada kilichogaiwa. Wengine walitengeneza mahema ya muda kutokana na mashuka yaliyofungwa kwenye miti, huku wengine wakisali wakiwa wamezungukwa na majengo yaliyoharibiwa na tetemeko.

Mmorocco aliyezaliwa Ujerumani Atik Azzouzi, mhandisi wa viwanda anayeishi Ujerumani, alikatisha likizo yake katika mji wa Nador ili kujitolea katika taasisi ya misaada ya Ujerumani kuja kuwasaidia wale wenye matatizo walioathiriwa na tetemeko la ardhi.

Waokoaji, wakisaidiwa na mbwa maalum, walipanda helikopta katika mji huo kuelekea kwenye zoezi jingine la uokoaji.

Waokoaji kutoka Uhispania, Uingereza na Qatar wanaendelea kuzisaidia timu za waokoaji wa Morocco, wakati Italia, Ubelgiji, Ufaransa na Ujerumani walisema misaada waliyoipendekeza inasubiri kuidhinishwa.

Idadi ya vifo kutokana na tetemeko la ardhi lililokuwa la kiwango cha 6.8 kwa kipimo cha rikta lililopiga katika milima ya High Atlas Ijumaa jioni imeongezeka na kufikia 2,901, huku watu waliojeruhiwa wameongezeka maradufu na kufikia 5,530, televisheni ya serikali iliripoti.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters.

Forum

XS
SM
MD
LG