Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 14:52

Uchaguzi Madagascar: Jeshi laonya dhidi ya jaribio lolote litakaloiyumbisha nchi


Askari wa Madagascar akitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji huko Antananarivo Oktoba 7, 2023. Picha na RIJASOLO/AFP.
Askari wa Madagascar akitumia vitoa machozi kuwatawanya waandamanaji huko Antananarivo Oktoba 7, 2023. Picha na RIJASOLO/AFP.

Jeshi la Madagascar limeonya dhidi ya jaribio lolote la kuiyumbisha nchi baada ya mwendesha mashitaka mkuu wa taifa hilo la kisiwa kutangaza kuwa maafisa wawili wamefunguliwa mashtaka ya kuchochea uasi kabla ya uchaguzi wa rais wa Novemba 16.

Wagombea kumi kati ya 12 wa upinzani walisusia kupiga kura kufuatia wiki kadhaa za maandamano ya ghasia mitaani. Tume ya uchaguzi ilimtangaza aliyekuwa madarakani Rais Andry Rajoelina kuwa mshindi, na mahakama ya kikatiba inatazamiwa kuidhinisha matokeo siku ya Ijumaa.

Mwendesha mashtaka, Narindra Rakotoniaina, alisema katika taarifa yake kwamba maafisa wawili wa jeshi walikuwa wamefungwa na wataendelea kuzuiliwa hadi kesi itakaposikizwa mnamo Januari 16. Hakuwataja maafisa hao wala kutoa vyeo vyao.

Akihutubia wanahabari katika mji mkuu wa Antananarivo siku ya Jumatano, Jenerali William Michel hakutaja kukamatwa kwa watu hao lakini alisema jeshi limejitolea kuheshimu matokeo ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG