Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 18, 2024 Local time: 13:53

Zoezi la kuhesabu kura za uchaguzi wa rais Madagascar linaendelea


Afisa wa uchaguzi Madagascar akionesha kura inayohesabiwa
Afisa wa uchaguzi Madagascar akionesha kura inayohesabiwa

Kura zinahesabiwa nchini Madagascar baada ya kufanyika uchaguzi wa rais uliosusiwa na idadi kubwa ya wapinzani.

Uchaguzi umefanyika baada ya wiki kadhaa za ghasia na maandamano, na katika mji mkuu wa Antananarivo wafuatiliaji wanasema uchaguzi umefanyika kwa amani lakini ni idadi ndogo ya wapiga kura waliojitokeza.

Upinzani ulitoa taarifa baada ya uchaguzi siku ya Alhamisi, inayosema kwamba idadi ya wapiga kura ilikuwa ndogo kabisa katika historia ya nchi hiyo, ikitaja takwimu za awali zilizotolewa na wafuatiliaji.

Maafisa wa uchaguzi wakitoa kura kutoka sanduka za kuweka kura wakianza utaratibu wa kuhesabu kura kutoikana na uchaguzi wa Novemba 16, 2023, mjini Antananarivo
Maafisa wa uchaguzi wakitoa kura kutoka sanduka za kuweka kura wakianza utaratibu wa kuhesabu kura kutoikana na uchaguzi wa Novemba 16, 2023, mjini Antananarivo

Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, CENI, inasema haina takwimu rasmi bado na hivyo haijtoa maoni yoyote kwa wakati huu.

Wapiga kura walionekana kwenye vituo vya kura katika maeneo yanayomunga mkono Rais Andry Rajoelina huku vituo kwenye mitaa ya upinzani vilikuwa kwa sehemu kubwa vitupu.

Vituo vilifungwa saa kumi na moja na matokeo ya awali yanatarajiwa kuanza kutolewa usiku.

Maafisa wa uchaguzi wanasema takwimu za awali za idadi ya wapiga kura waliojitokeza maeneo ya chama tawala ilifikia asili mia 30 na ilikuwa kati ya asili mia 15 hadi 20 katika maeneo ya upinzani, hiyo ikiashiria kwamba watu huenda wamechukizwa na uchaguzi huo.

Forum

XS
SM
MD
LG