Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:06

Marekani yaipongeza Poland kwa kuimarisha uhuru wake


Rais Donald Trump akiwa na Rais wa Poland Andrzej Duda. Mke wa Trump Melania yuko pamoja nao.
Rais Donald Trump akiwa na Rais wa Poland Andrzej Duda. Mke wa Trump Melania yuko pamoja nao.

Rais wa Marekani Donald Trump ameipongeza Poland kwa mfano katika kuimarisha uhuru wao.

Trump akiwa Poland alisema anapenda “kulitolea mfano taifa hilo kuwa ni kigezo kwa wengine ambao wanatafuta uhuru wao na anapenda kutoa wito wa kuwapa moyo na utayari kutetea ustaarabu wetu.”

Alisema Alhamisi kwamba sababu ya ziara yake Poland ilikuwa ni pamoja na mambo mengine kumtembelea mshirika wa Marekani.

Hotuba yake huko Warsaw katika eneo la Krasinski ilikuwa ni ya kwanza huko Ulaya, na ilifanyika katika eneo ambalo lililokuwa na alama ya utaifa wa watu wa Poland, wakiadhimisha kusimama kwao imara dhidi ya utawala wa mabavu.

“Simulizi ya Poland ni habari ya watu ambao hawajakata tamaa, hawajawahi kuvunjika moyo na hawajasahau wao ni taifa la namna gani,” Trump amesema.

Rais wa Marekani amesema mapema Alhamisi katika mkutano wa pamoja na Rais wa Poland Andrzej Duda kwamba Marekani inashirikiana na Poland kutafuta ufumbuzi wa “vitendo na tabia ya hujuma” ya Russia, akiongeza kuwa Marekani imejizatiti kuhakikisha amani na usalama wa upande wa mashariki na kati mwa Ulaya.

Pia Trump ameipongeza Umoja wa Kujihami wa Ulaya (NATO) kuwa ni muhimu katika kudhibiti migogoro.

Amewalaumu baadhi ya wanachama wa NATO kwa kutolipa michango yao kwa kiwango kinachotakiwa kwa ajili ya jeshi lao, na Alhamisi alisema Poland ni mshirika pekee ambaye anatekeleza majukumu yake ya malipo kikamilifu

XS
SM
MD
LG