Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:08

Zelensky asisitiza kuundwa mahakama maalum kushughulikia uhalifu wa Russia


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy

Rais wa Ukraine volodymir zelensky amesema leo kwamba mahakama maalumu lazima iundwe ili kuiwajibisha Russia kwa uhalifu wa uchokozi wake.

“Ni vyema kuwepo na uwajibikaji kwa uhalifu huu. Hili linaweza tu kuimarishwa na mahakama,” aliwaambia wanadiplomasia na maafisa katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu huko The Hague, ambayo ilitoa hati ya kukamatwa kwa Vladimir Putin kwa uhalifu vita.

Rais wa Ukraine alitembelea ICC huko Uholanzi leo katika ziara ya kushtukiza The hague. Nje ya jengo la ICC bendera ya Ukraine ilipanidhswa karibu na bendera ya ICC.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy anaeleza: “ Ni taasisi moja ndio yenye uwezo wa kujibu kuhusu uhalifu , uhalifu wa uchokozi, katika mahakama. Mahakama siyo kitu cha mseto kinachoweza kufunga mada rasmi. Sio maelewano ambayo yatawaruhusu wanasiasa kusema kwamba kesi inatuhumiwa kufanyika, lakini ukweli, ya kweli yenye ahadia kamili. Kweli na haki kamili.”

ICC katika taarifa yake ya March 18 ilisema kwamba Putin anadaiwa kuhusika na uhalifu wa kivita wa kuwafukuza watoto kinyume cha sheria kutoka maeneo yanayokaliwa kwa mabavu na Ukraine hadi Russia.

Zelenskyy: “ tafadhali pia kumbuka wa- ukraine, wanaume, wanawake, watu wazima, watoto nani angekuwa mzima leo, lakini kwa uchokozi huu. Vita ambayo hatukuvitaka, ila tunapaswa kuvifanya vya mwisho na tutafanya. Ushindi kwa ukraine.”

XS
SM
MD
LG