Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 23:56

Russia yasema Marekani ilihusika na shambulizi la droni huko Kremlin


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Russia Alhamisi imeishutumu Marekani kwa kuhusika na shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani dhidi ya Kremlin.

Kremlin imesemana kuwa mashambulizi ya hujuma yanayofanywa na Ukraine katika maeneo ya Russia yamefikia kiwango kisichokuwa cha kawaida.

Russia imesema Ukraine imefanya shambulizi la ndege mbili zisizokuwa na rubani yenye lengo la kumuuwa rais Vladmir Putin, shutuma ambazo Kyiv imezikanusha.

“Maamuzi kwa mashambulizi kama hayo hayafanyiki Kyiv, lakini ni Washington , amesema msemaji wa Kremlin Dmitry Peskov. Kyiv inafanya kile ilichoambiwa ifanye.

“ Washington inatakiwa kuelewa hili wazi kwamba tunajua,” alisema.

Peskov alisema Putin alikuwa akifanya kazi katika ofisi yake huko Kremlin kama kawaida siku ya Alhamisi lakini akaongeza kuwa hatua za usalama Moscow zitaimarishwa kufuatia shambulio hilo, ambalo Kremlin ilisema lilitokea usiku kati ya jumanne na jumatano

Russia pia imeripoti mfululizo wa mashambulizi ya ndege zisizokuwa na rubani katika vituo vya mafuta na njia za reli ikiilaumu Ukraine.

XS
SM
MD
LG