Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 23:35

Zambia yasherehekea makubaliano yaliyofikiwa ya muundo wa deni lake la takriban dola za Kimarekani bilioni 6.3


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema.

Zambia ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiafrika kushindwa kulipa deni lake wakati wa janga la virusi vya corona na wachambuzi wanasema makubaliano hayo yanafungua njia kwa nchi zinazoendelea kukumbwa na matatizo madeni.

Wabunge nchini Zambia walikuwa katika hali ya furaha sana siku ya Ijumaa walipokuwa wakiimba wimbo wa taifa wakati wa kikao cha bunge, na kuweka kando ushirika wao wa kisiasa kusherehekea makubaliano hayo.

Spika wa Bunge la Taifa Nelly Mutti aliwapongeza wabunge bungeni kwa kuimba wimbo wa taifa kwa hamasa na nguvu. Alitania kwamba hata kiongozi wa upinzani alijiunga katika shamra shamra.

Wananchi wa Zambia kote nchini humo, pamoja na kwenye mtandao, walijiunga katika shamra shamra hizo.

Waziri wa Ulinzi wa Zambia Ambrose Lufuma alikaribisha kufanyiwa makubaliano ya muundo wa deni wakati alipozungumza na wabunge katika bunge siku ya Ijumaa na kumpongeza rais wa nchi Hakainde Hichilema.

Waziri wa Ulinzi Lufuma, “Ni makubaliano yamekamilika. Bahati nzuri tuna kiongozi mwenye mtizamo, kiongozi mwenye nia ya dhati, kiongozi mwenye mapenzi, ambaye alipitia magumu mengi sana.”

Rais Hichilema alisema kwenye Twitter Alhamisi kwamba makubaliano ni hatua kubwa ya kihistoria katika safari ya nchi kuelekea katika kufufua na kukua kwa uchumi.

Katika taarifa iliyotolewa mjini Lusaka siku ya Alhamisi, Waziri wa Fedha Felix Nkulukusa alisema, chini ya makubaliano, wakopeshaji rasmi watatoa mpango wa muundo kwa deni ambalo Zambia inalo mwishoni mwa program ambayo inafadhiliwa kifedha.

Waziri Felix Nkulukusa wa kwanza kutoka kushoto akishiriki katika mazungumzo ya IMF, Washington, DC, Marekani Aprili 12, 2023. REUTERS/Ken Cedeno
Waziri Felix Nkulukusa wa kwanza kutoka kushoto akishiriki katika mazungumzo ya IMF, Washington, DC, Marekani Aprili 12, 2023. REUTERS/Ken Cedeno

Nkulukusa alisema misingi ya makubaliano yataelezewa na kurasmishwa katika waraka wa maelewano kati ya Zambia na wakopesha wake rasmi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Fedha, Kristalina Georgieva, katika taarifa yake, aliipongeza Zambia kwa makubaliano hayo.

FILE PHOTO: Kristalina Georgieva
FILE PHOTO: Kristalina Georgieva

Ikiwa imefanikiwa kuweka muundo mzuri wa deni lake ina maana kuwa Zambia itakuwa na uwezo wa kupatiwa dola milioni 188 kutoka IMF.

Afisa mwandamizi wa uchumi wa chama cha Uchumi cha Zambia Trevor Simumba aliiambia VOA kwamba makubaliano hayo ni mabadiliko kwa Zambia.

Simumba alisema hivi sasa kazi ngumu ndiyo inaanza kupata dola bilioni 6.8 ambazo ni za ziada na wakopeshaji binafsi

Simumba amesema “ni hatua muhimu sana. Inaonyesha kwamba jumuiya ya kimataifa kwa asilimia 100 iko nyuma ya Zambia, nadhani ni habari nzuri kwa Zambia. Kilicho muhimu hivi sasa ni kuelewa kwamba kutakuwa na kazi nyingi sana za kufanya ambazo zimeshughulikia kwa kina katika makubaliano.”

Wizara ya Fedha inasema Zambia inadaiwa na China zaidi ya dola bilioni 6, wakati wakopeshaji wengine wanawadai dola bilioni 3.5.

Takwimu za serikali zinaonyesha deni la kigeni la Zambia kwa jumla hadi kufikia mwisho wa mwaka 2022 lilikadiriwa kuwa katika kiwango cha dola bilioni 18.6.

Forum

XS
SM
MD
LG