Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Oktoba 09, 2024 Local time: 04:36

Zambia : Hichilema amateua mtaalam wa uchumi kuwa Waziri wa Fedha


Rais wa Zambia Hakainde Hichilema
Rais wa Zambia Hakainde Hichilema

Rais mpya wa Zambia Hakainde Hichilema amemteua mtaalamu wa uchumi wa kimataifa mwenye ujuzi kuwa Waziri wa Fedha.

Mtaalamu huyo amekabidhi jukumu kubwa la kuliokoa taifa hilo kutoka mizozo miwili ya madeni na fedha.

Uteuzi wa Situmbeko Musokotwane aliyewahi kushika nyadhifa hiyo kuanzia 2008 hadi 2011 umetangazwa leo.

Uteuzi wa Musokotwane umekuja siku tatu baada ya Rais Hichilema kuahidi wakati wa kuapishwa kwake kwamba atafanya kila njia kudhibiti tena matumizi ya umaa na nakisi katika bajeti.

Mbali na kutayarisha sera za kubana matumizi Musokotwane, aliyewahi kuwa Gavana wa benki kuu pamoja na kuwa na nyadhifa muhimu kwenye Benki Kuu ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha Duniani (IMF), atakabiliwa na majadiliano magumu na wakopeshaji mbali mbali wakigeni wanoaidai nchi hiyo ya kusini mwa Afrika karibu dola bilioni 12.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali

XS
SM
MD
LG