Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 16:09

Rais mpya wa Zambia aapishwa


Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema.
Rais mteule wa Zambia Hakainde Hichilema.

Kiongozi aliyechaguliwa hivi karibuni wa Zambia Hakainde Hichilema anaingia madarakani Jumanne baada ya ushindi mkubwa  wa uchaguzi

Kiongozi aliyechaguliwa hivi karibuni wa Zambia Hakainde Hichilema anaingia madarakani Jumanne baada ya ushindi mkubwa wa uchaguzi uliosifiwa kama ushindi wa nadra juu ya utawalla wa kiimla na hatua muhimu katika demokrasia ya Afrika.

Hichilema, mwenye umri wa 59, atakula kiapo mbele ya umati ambao utajumuisha wanasiasa wa upinzani kutoka nchi za kanda hiyo na vile vile viongozi wa sasa na wa zamani wa Afrika.

Maelfu ya watu walilala ndani ya Uwanja wa Mashujaa katika mji mkuu Lusaka, ambapo sherehe hiyo ilianza Jumanne asubuhi, ili kuhakikisha kuwa na kiti, alisema mpiga picha wa video wa AFP katika eneo hilo.

Katika jaribio lake la sita la kugombea urais, Hichilema alimshinda Edgar Lungu, mwenye umri wa miaka 64, kwa kura karibu milioni moja kuanguka huko kulisababishwa na ugumu wa uchumi na vizuizi vya uhuru chini ya utawala uliopita.

Ushindi huo ni wa 17 wa upinzani Kusini mwa Jangwa la Sahara tangu mwaka 2015.

Ilitokea licha ya kuzuia kampeni na kushukiwa na wizi wa kura kwa kupendelea chama cha Lungu.

Ilitokea licha ya kuzuia kampeni na kushukiwa wizi wa kura kwa kupendelea chama cha Lungu.

Idadi ya wapiga kura Agosti 12 ilikuwa karibu asilimia 71, na Wazambia wengi walipiga foleni hadi usiku kupiga kura zao.

XS
SM
MD
LG