Wapiganaji wa IS Januari walifanya shambulizi lao kubwa ambalo halijawahi kutokea kwa miaka kadhaa katika jela ya Ghwayran katika mji unaodhibitiwa na Wakurdi wa Hasakeh kwa lengo la kuwaachia huru wapiganaji wenzao na wengine kadhaa.
Idadi ya vifo katika mapigano makali tangu wakati huo imeongezeka na kufikia 332 wakati vikosi vya Syria Democratic Forces vinavyoungwa mkono na Marekani vikipata zaidi ya miili 50 usiku wa kuamkia leo katika majengo ya gereza na maeneo ya karibu, shirika linalofuatilia haki za binadamu nchini Syria limesema.
Kundi hilo lenye makao yake makuu ambalo linategemea vyanzo ndani vya Syria limesema kuwa wana jihadi 246, wapiganaji wa Kikurdi 79 na raia wengine saba wameuawa hadi sasa katika mashambulizi ya IS na mapigano mengine.
SDF ilitangaza kuwa imechukua udhibiti wa jela hiyo Jumatano lakini mapigano makali yaliendelea hadi Jumamosi kati ya wapiganaji wa kikurdi na wanajihadi karibu na gereza hilo.
Kwa mujibu wa SDF takriban wafungwa 3,500 na wapiganaji wa IS wamejisalimisha kwa vikosi vyake tangu operesheni zilipoanza tena jela.
Lakini maafisa wa Kikurdi wanakadiria kwamba kati ya wapiganaji wa IS 60 na 90 walikuwa wanashikiliwa katika jela hiyo.