Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 10:48

Shambulizi la Marekani lamuua kiongozi wa juu wa al-Qaida Syria


Ndege aina ya MQ-9 Reaper.

Kiongozi wa ngazi ya juu wa al-Qaida ameuawa katika shambulizi la ndege isiyokuwa na rubani nchini Syria, Wizara ya Ulinzi ya Marekani imesema Ijumaa.

Shambulizi hilo limefanyika siku mbili baada ya kituo cha kijeshi kusini mwa Syria kinachotumiwa na ushirika unaongozwa na Marekani unaopambana na kikundi cha Islamic State kushambuliwa.

“Shambulizi la anga la Marekani lilifanyika leo huko kaskazini magharibi mwa Syria na kumuua kiongozi wa ngazi ya juu wa al-Qaida Abdul Hamid al-Matar,” taarifa ya msemaji wa kikosi cha Central Command Meja wa Jeshi John Rigsbee imeeleza.

Hapakuwa na vifo vya raia vilivyojulikana kutokana na shambulizi hilo, amesema, akiongeza lilifanyika kwa kutumia ndege aina ya MQ-9.

“Kuuawa kwa kiongozi huyu wa ngazi ya juu wa al-Qaida kutavuruga uwezo wa taasisi ya kigaidi katika kupanga na kutekeleza mashambulizi yake ulimwenguni,” amesema.

Mwishoni mwa mwezi Septemba Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilitangaza imemuua Salim Abu-Ahmad, kamanda mwingine wa juu wa al-Qaida huko Syria, katika shambulizi la anga karibu na Idlib mji ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Alikuwa anahusika katika “kupanga, kufadhili na kuidhinisha mashambulizi ya kikanda yanayofanywa na al-Qaida, kulingana na Centcom.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG