Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 11:59

Yates aliitahadharisha White House kuhusu Flynn


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa James Clapper (K) akiwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani Sally Yates
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa James Clapper (K) akiwa na Mwanasheria Mkuu wa zamani Sally Yates

Aliyekuwa kaimu Mwanasheria Mkuu wa Marekani Sally Yates amesema Jumatatu kwamba alikuwa ameitahadharisha ikulu ya White House kuwa Jenerali Michael Flynn anaweza kudhibitiwa na Russia.

Yates ameeleza kuwa alisema hilo mwanzoni tu Rais Donald Trump alipochukua madaraka na kumteua Flynn, ambaye ni Jenerali mstaafu, kuwa mshauri wake wa usalama wa taifa.

Yates ameliambia jopo la Baraza la Seneti kuwa aliwatahadharisha ikulu ya White House wiki mbili kabla ya Trump kumfukuza Flynn kwa kudanganya kuhusu mawasiliano yake na balozi wa Russia nchini Marekani.

Amesema kuwa alikuwa ana wasiwasi kuhusu matamko yaliyojirejea ya Makamu wa Rais Mike Pence na viongozi wengine yakipotosha kuwa Flynn hakuwa na mawasiliano na balozi Sergey Kislyak, wakati uchunguzi wa kawaida ulikuwa umeonyesha kuwa watu hao walikuwa wanafanya mazungumzo.

“Makamu wa Rais na wengine walikuwa wanawajibu kujua kwamba taarifa walizokuwa wanatoa kwa wananchi wa Marekani zilikuwa sio za kweli,” Yates amesema.

Na Russia ilikuwa inajua lile ambalo Jenerali Flynn alikuwa amefanya, na Russia ilikuwa inafahamu kuwa Jenerali Flynn alikuwa anampotosha makamu wa rais.”

Ameongeza kuwa, “Kila mara hilo lilipotokea, lilikuwa linaongeza uwezekano wa kudhibitiwa, na kusema lililo wazi, hutotaka mshauri wa usalama wa taifa wa serikali yako adhibitiwe na Russia.

Siku 18 baada ya Yates kuwasilisha wasiwasi wake ikulu ya White House, Trump alimfukuza kazi Flynn, akisema kuwa hana imani naye kushika nafasi hiyo nyeti ya ikulu ya White House kama mshauri wake

XS
SM
MD
LG