Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 06:57

Marekani yasitisha misaada kwa wizara ya Afya Kenya


Rais Donald Trump wa Marekani.
Rais Donald Trump wa Marekani.

Balozi wa Marekani nchini Kenya, Robert Godec, Jumanne alitangaza kwamba serikali yake imesitisha kwa muda misaada inayotoa kwa wizara ya afya nchini humo, hadi pale masharti fulani yatakapotimizwa.

Alisema misaada hiyo ni pamoja na ile inayotolewa kupitia shirika la maendeleo ya kimataifa (USAID).

Godec aliiandikia barua wizara ya afya na kueleza sababu zilizopelekea hatua hiyo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation, Godec amesema serikali ya Marekani imechukua hatua hiyo kwa sababu ya ripoti nyingi za matumizi mabaya ya fedha, na ufisadi.

Alisema anna wasiwasi na uhasibu unaofanyawa na wizara ya afya na kwamba huenda misaada isiwafikie wale waliokusudiwa.

Hata hivyo, waziri wa Afya nchini Kenya, Cleopas Mailu, katika taarifa kwa vyombo vya habari Jumanne, alisema kuwa wizara yake inayashughulikia masharti iliyopewa na Marekani na kwamba baadhi ya programu hazikuathiriwa na usitishwaji huo wa misaada.

Shirika la misaada ya kimataifa, USAID, liliwaalika wadau wote na kuwaalika kwa mkutano utakaofanyika Jumatano mjini Nairobi, ili kuelezewa kwa kina kuhusu hatua hiyo ya serikali ya Marekani.

Akizungumza na idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika kwa njia ya simu, afisa mmoja wa uratibu wa programu za USAID nchini Kenya, Sonia Gloss, alisema kuwa wadau hao watafahamishwa kwa kina zaidi kuhusu kisa na maana ya hatua hiyo ya serikali ya Marekani.

Haya yanajiri baada ya utawala wa Trump kuwasilisha bungeni makadirio ya matumizi ya fedha za serikali ambayo yanagharamia ufadhili wa programu za misaada kwa kiasi cha takriban dola bilioni moja hadi mwezi Septemba, 2017.

XS
SM
MD
LG