Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Juni 18, 2024 Local time: 23:55

WHO: Si sahihi kufikiria kuenea kwa omicron ni mwisho wa COVID-19


Tedros Adhanom Gebreyesus
Tedros Adhanom Gebreyesus

Mkuu wa Shirika la Afya Duniani - WHO amesema Jumatatu itakuwa hatari kufikiria kirusi kinachoenea kwa kasi cha omicron ni cha mwisho na kwamba dunia imefikia mwisho wa janga la COVID-19.

Badala yake Tedros Adhanom Gebreyesus amesema kuna uwezekano mwaka 2022 kuondoka katika awamu kali ya janga hilo ambapo COVID-19 imekuwa dharura ya afya duniani.

Amesema hilo linaweza kufikiwa iwapo mikakati na zana kama vile upimaji na chanjo vinatumika kwa njia ya kina.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano wa Bodi ya Utendaji, Tedros amesema tangu Omicron kutambuliwa kwa mara ya kwanza zaidi ya wiki tisa zilizopita zaidi ya kesi milioni 80 ziliripotiwa kwa shirika hilo la Umoja wa Mataifa, zaidi ya ilivyoripotiwa mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG