Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 24, 2024 Local time: 09:58

Wataalam wahimiza uendelezaji chanjo pamoja na hali ya maambukizi kupungua Afrika


Kijana akiwa na familia yake katika kituo cha chanjo cha Discovery wakati akisubiri kudungwa chanjo Pfizer/BioNTech dhidi ya COVID-19 huko Sandton, Johannesburg, Dec. 15, 2021.(Photo by LUCA SOLA / AFP).
Kijana akiwa na familia yake katika kituo cha chanjo cha Discovery wakati akisubiri kudungwa chanjo Pfizer/BioNTech dhidi ya COVID-19 huko Sandton, Johannesburg, Dec. 15, 2021.(Photo by LUCA SOLA / AFP).

Wimbi la nne la maambukizi ya virusi vya Corona Afrika linaripotiwa kupungua lakini wanasayansi wanasema ipo haja kubwa sana ya kuendelea kutoa chanjo kwa watu.

Katika taarifa, shirika la afya duniani limesema kwamba kiwango cha maambukizi ya virusi vya Corona hakijabadilika kwa muda wa siku saba kufikia Januari tarehe 9.

Afrika Kusini, ambako maambukizi mengi yameripotiwa Afrika, imeripoti kwamba maambukizi yamepungua kwa asilimia 14.

Shirika la Afya Duniani limesema kwamba maambukizi ya corona nchini Afrika kusini, ambapo virusi vya Omicron viligunduliwa, yamepungua kwa asilimia 9. Maambukizi pia yamepungua katika nchi za Afrika mashariki na kati.

Maambukizi hata hivyo yameongezeka katika nchi za Afrika kaskazini kwa asilimia 121.

Maambukizi pia yameongezeka Afrika Magharibi katika kipindi cha wiki moja iliyopita.

Dkt Abdou Salam Gueye, mkuu wa idara ya kusimamia majanga barani Afrika katika shirika la WHO amesema imechukua muda mfupi kwa Omicron kusambaa sana ikilinganishwa na Delta.

Dkt Gueye anaeleza: "Kufikia sasa, nchi 30 za Afrika zimegundua na kuripoti maambukizi ya Omicron. Katika nchi ambazo maambukizi yamesambaa sana, Omicron imegunduliwa sana na kwa haraka. Ilichukua muda wa wiki mbili kwa Delta kwa kulinganisha, ilichukua Delta wiki nne kufikia Beta katika viwango vya maambukizi

XS
SM
MD
LG