Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 20:57

WHO kuzindua chanjo ya homa ya manjano


Shirika la Afya Duniani 'WHO' litazindua hii leo Alhamisi kampeni ya chanjo ya dahrura dhidi ya homa ya manjano, maarufu Yellow Fever, kwenye mpaka kati ya Angola na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

WHO inasisitiza kwamba kuzuia uenezaji wa ugonjwa huo duniani ndio kipaombele kuu cha wakati huu.

Kampeni hiyo itaanza Julai hasa kwa kuzingatia maeneo ya mpakani ambako kuna shughuli nyingi za kibiashara. Kulingana na WHO, kampeni hiyo itafanyika kwenye mpaka huo wenye urefu wa kilomita 75-100 na pia maeneo ya mji ya Kinshasa kwa lengo la kuunda eneo la kinga dhidi ya kirusi cha homa hiyo ili kuzuia kuenea kimataifa.

Kufikia mwezi huu, nchi za China, Kenya na DRC zimeripoti kesi za homa ya manjano zinazohusishwa na mlipuko ulotokea Angola.

XS
SM
MD
LG