Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 11, 2024 Local time: 02:27

WFP yaongeza msaada kwa kiasi kikubwa katika mpaka wa Chad na Sudan kukabiliana na mahitaji ya wakimbizi


FILE PHOTO: Mtu akipita eneo lililoshambuliwa kwa mabomu mjini Kaskazini ya Khartoum.
FILE PHOTO: Mtu akipita eneo lililoshambuliwa kwa mabomu mjini Kaskazini ya Khartoum.

Shirika la chakula duniani – WFP limesema linaongeza msaada wake kwa kiasi kikubwa katika eneo la mpaka wa Chad na Sudan.

Imeeleza inachukua hatua hiyo ili kusaidia maelfu ya watu wanaokimbia mapigano baina ya makundi mawili ya jeshi la Sudan.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa limesema takriban watu laki mbili wamekimbia Chad tangu ghasia zilipoanza April mwaka huu.

Wiki iliyopita pekee, watu elfu 20 wamevuka mpaka kutoka mkoa wa Darfur hadi mpaka wa Chad katika mji wa Adre.

FILE - Wakimbizi wakusanyika eneo la hospitali ya Adre, Chad Juni16, 2023 . ( Courtesy of Mohammad Ghannam/MSF/Handout via REUTERS)
FILE - Wakimbizi wakusanyika eneo la hospitali ya Adre, Chad Juni16, 2023 . ( Courtesy of Mohammad Ghannam/MSF/Handout via REUTERS)

WFP imesema wengi wanawasili wakiwa wamejeruhiwa vibaya. Kuna taarifa kwamba raia wanaokimbia wanalengwa makusudi, kukiwa na dalili za vita vya kikabila katika vurugu hizo.

Mapema shirika la kutetea haki za binadamu- Human Rights watch, lilitoa wito kwa mahakama ya kimataifa ya uhalifu kufanya uchunguzi wa uhalifu wa vita uliofanyika mkoa wa Darfur magharibi mwa Sudan, ikiwemo mauaji ya dazani za raia.

Forum

XS
SM
MD
LG