Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 21:31

RSF yatuhumiwa kufanya shambulizi


Watu wenye silaha kutoka kikosi cha dharura RSF cha Sudan, walituhumiwa kushambulia mji wa mbali Ijumaa kabla ya kufanya mashambulizi ya risasi na uporaji ambao mashahidi walisema uliwatia hofu watu.

Kwa karibu miezi mitatu, RSF inayoongozwa na Mohamed Hamdan Daglo imepigana na jeshi chini ya Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, katika vita vilivyogharimu maisha ya watu 3,000 na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

RSF ilikuwa ikipora benki na majengo ya umma huko Bara, kilomita 50 kaskazini mashariki mwa El-Obeid, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini, shahidi katika mji huo amesema.

Mapigano hayo tangu Aprili 15 yamejikita katika mji mkuu Khartoum pamoja na Kordofan Kaskazini na eneo kubwa la magharibi la Darfur, ambapo Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu uwezekano wa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Forum

XS
SM
MD
LG