Mkurugenzi wa WFP, David Beasleg, ambaye ametembelea jimbo hilo hivi karibuni, amesema kwamba bila ya kuwa na msaada wa dharura, zaidi ya watu nusu milioni watalazimika kuanza kuomba chakula cha msaada.
Pia Beasleg ameongeza kuwa watu wengine 800,000 wanaelekea kukabiliwa na hali hiyo.
WFP imesema hali hiyo imesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi, na kutokea ukame mfululizo ambao umelazimisha familia kushindwa kujitegemea.
Mkurugenzi huyo wa WFP amesisitiza kwamba mataifa tajiri yana wajibu wa kusaidia.