Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 13:12

Kura zaanza kuhesabiwa katika baadhi ya majimbo Ethiopia


Raia wa Ethiopian katika vituo vya kuoigia kura katika mji wa Debre Birhan, Ethiopia.
Raia wa Ethiopian katika vituo vya kuoigia kura katika mji wa Debre Birhan, Ethiopia.

Wapiga kura katika mkoa wa Sidama nchini Ethiopia wamejitokeza kwenye vituo vya kupigia kura wakati maafisa wameanza kuhesabu kura katika majimbo mengine kwa uchaguzi uliofanyika jumatatu ambao uligubikwa na kususiwa na upinzani, vita, na ripoti za kasoro katika baadhi ya maeneo.

Waziri mkuu Abiy Ahmed anatumai chaguzi hizo kwenye ngazi ya kitaifa na majimbo zitaonyesha ufanisi wa mageuzi ya kidemokrasia aliyoanzisha baada ya kuteuliwa na muungano wa vyama tawala mwaka 2018.

Lakini uchaguzi huo umeonyesha pia hali mbaya inayojiri katika taifa hilo lenye watu millioni 109, mamlaka jumatatu haikuweza kuandaa uchaguzi katika majimbo manne kati ya 10, likiwemo jimbo la Sidama, ambapo kuliripotiwa matatizo ya vifaa kwa mujibu wa tume ya uchaguzi.

Abiy alisema jana katika taarifa “ demokrasia haijengwi kwa siku moja. Tunaweka tofali kwa tofali.”

Katika majimbo mawili ambako uchaguzi ulifanyika, imeripotiwa kwamba waangalizi wa upinzani walifukuzwa kwenye vituo vingi vya kupigia kura, kiongozi wa tume ya uchaguzi Birtukan Midekssa aliwaambia waandishi wa habari jana.

XS
SM
MD
LG