Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 16, 2024 Local time: 18:56

Waziri wa Afya wa Uingereza atahadharisha kusambaa kwa kasi kwa Omicron


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akitembelea kituo cha kutoa chanjo mjini London.
Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akitembelea kituo cha kutoa chanjo mjini London.

Waziri wa Afya wa Uingereza Sajid Javid amesema kwamba aina mpya ya virusi vya Corona Omicron, inasambaa kwa kasi sana nchini Uingereza na kuweka mazingira ambapo virusi hivyo vinashindana na chanjo.

Sajid Javid
Sajid Javid

Akizungumza katika mahojiano kwenye televisheni ya Sky News, Javid amekariri tangazo la serikali ya Uingereza kwamba vituo vya kutoa chanjo vitafunguliwa kila siku hata siku za likizo, ili kuongeza kasi ya watu kupata chanjo ya ziada inayoimarisha kinga dhidi ya virusi vya Corona.

Waziri wa Afya wa Uingereza amesema : "Kile tumejifunza kutokana na aina mpya ya virusi vya Corona - Omicron, katika wiki moja ya maambukizi ni kwamba vinasambaa kwa kasi sana. idadi ya watu wanaoambukizwa inaongezeka zaidi ya mara mbili kila baada ya siku mbili au tatu. Tunatarajia kwamba kutatokea wimbi kubwa la maambukizi. Kitu kingine ambacho tumegundua ni kwamba dozi mbili za kwanza hazitoshi kukulinda, dozi ya tatu ya kuimarisha king ani muhimu sana kukulinda dhidi ya maambukizi yasiyokuwa na dalili.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ametangaza kwamba serikali itazindua kampeni ya dharura ya utoaji wa chanjo ya tatu ili kudhibithi maambukizi na kuzuia vifo kutokana na wimbi la maambukizi.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameeleza : "Nina wasiwasi kwamba tunakabiliana na hali ya dharura katia vita vyetu dhidi ya Omicron na tunastahili kuchukua hatua za haraka kutoa chanjo ili kuwalinda marafiki wetu na watu tunaowapenda.

Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Mapema hii leo maafisa wanne wa ngazi ya juu wanaosimamia matibabu nchini Uingereza wametangaza hali ya tahadhari ya juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya COVID. Ushahidi unaonyesha kwamba maambukizi ya Omicron yanaongezeka mara mbili hapa Uingereza kila baada ya siku mbili au tatu. Hakuna mtu anayestahili kuwa na shauku kwa hili kwamba kuna maambukizi ya Omicron yanayosambaa kwa kasi sana. Nina hofu kwamba dozi mbili za chanjo hazitoshi kutulinda dhidi ya maambukizi."

XS
SM
MD
LG