Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 11:30

Waziri wa Afya Uingereza ajiwekea karantini baada ya kukutikana na maambukizi


 Waziri wa Afya wa Uingereza Nadine Dorries
Waziri wa Afya wa Uingereza Nadine Dorries

Wakati Waziri wa Afya Uingereza Nadine Dorries amethibitishwa Jumatano kuambukizwa virusi vya corona.

Dorries amechukuwa tahadhari zote na kujitenga na watu wengine, kwa kujiwekea karantini nyumbani kwake.

Hali hii imekuja wakati kukiwa na taarifa ya kifo cha mtu wa sita aliyekuwa na maambukizo ya virusi vya corona ambapo hadi sasa watu 382 wameambukizwa.

Mtu aliyefariki hivi karibuni ni mzee mwenye umri wa miaka 80 ambaye alikuwa ana mgogoro wa kiafya.

Naye Gavana wa New York Andrew Cuomo, ametangaza kwamba wanajeshi watapelekwa katika mji wa New Roshell, ulio kaskazini mwa jimbo hilo, katika juhudi za kuzuia virusi vya Corona kusambaa.

Jeshi la kitaifa litapeleka vyakula kwa watu ambao wamewekwa chini ya uangalizi.

Sehemu hiyo ni ya hivi punde kuripoti maambukizi ya juu ya virusi vya Corona nchini Marekani.

Nchini Afrika kusini, watu wengine sita wamethibitishwa kuambukizwa Corona na kufikisha idadi ya maambukizi kuwa watu 13.

Maambukizi mapya yameripotiwa katika mikoa ya Gauteng, Kwa zulu Natal, na Western cape.

Walioambukizwa ni watu waliorejea kutoka Ulaya hivi karibuni.

Serikali ya Afrika kusini imetuma ndege kuwachukua zaidi ya raia wake 120 waliokwama Wuhan, China kufuatia mlipuko wa Corona.

Inatarajiwa kurudi Afrika kusini, kesho kutwa ijumaa, katika safari itakayogharimu dola milioni 1.6.

Nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, mgonjwa aliyethibitihswa kuambukizwa Corona ametengwa na anaendelea kupokea matibabu, akifikisha idadi ya maambukizi kusini mwa jangwa la sahara kuwa watu saba.

Mgonjwa huyo, raia wa DRC anayeishi Ufaransa, alirudi Congo wiki hii, March 8, na hakuonyesha dalili za maambukizi ya Corona.

Watu wengine waliokuwa na mgonjwa huyo, nao wametengwa.

XS
SM
MD
LG