Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 15, 2024 Local time: 06:20

Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edward Lowassa afariki akiwa na umri wa miaka 70


Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edwars Lowass (kulia).
Waziri Mkuu wa zamani wa Tanzania Edwars Lowass (kulia).

Waziri mkuu wa zamani wa Tanzania, Edward Lowassa, alifariki Jumamosi katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Dar es Salaam akiwa na umri wa miaka sabini.

Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia televisheni ya Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC), makamu wa rais wa nchi hiyo, Dk Philip Mpango, alisema Lowassa alifariki baada ya kuugua magonjwa ya kujikunja utumbo, matatizo ya mapafu na shinikizo la damu.

“Hayati Edward Lowassa ameugua kwa muda mrefu na amekuwa akipatiwa matibabu tangu Januari 14, 2022 JKCI na baadaye akapelekwa kwa matibabu zaidi nchini Afrika Kusini na kurejea tena JKCI,” alisema Dkt Mpango.

Lowassa aliyezaliwa Agosti 26, 1953, alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 1974–1977 na kuhitimu Shahada ya Sanaa katika Elimu na baadaye Chuo Kikuu cha Bath, Uingereza kwa Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Maendeleo (mwaka 1983–1984).

Baada ya kumaliza chuo kikuu, Lowassa alifanya kazi ndani ya CCM akiwa ofisa wa ngazi ya juu kuanzia wilaya, mkoa na baadaye makao makuu kati ya mwaka 1977–1989.

Mnamo mwaka 2005, Rais Jakaya Kikwete alimteua kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Bunge likamthibitisha.

Uwaziri mkuu wa Lowassa ulifika mwisho Februari 2008, alipojiuzulu kutokana na kashfa ya Richmond.

Lowassa, kwa tikiti ya chama cha Chadema, alikuwa mpinzani mkuu wa John Magufuli wa chama cha CCM katika uchaguzi wa rais wa 2015 ambapo Magufuli alishinda.

Forum

XS
SM
MD
LG