Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 22:54

Tanzania: Waziri wa Katiba na Sheria Augustine Mahiga afariki


Dr Mahiga

Waziri wa Katiba na Sheria wa Tanzania Dkt Augustine Mahiga aliaga dunia Ijumaa akiwa nyumbani kwake Dodoma, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasililiano ya Ikulu.

Mahiga alikuwa na umri wa miaka 74.

"Mhe. Balozi Mahiga ameugua ghafla akiwa nyumbani kwake jijini Dopdoma na amefikishwa hospitali akiwa tayari amefariki dunia," ilieleza taarifa ya ikulu.

Katika salamu zake za rambirambi, Rais John Magufuli alimtaja Mahiga kama afisa mchapakazi na mwenye unyenyekevu.

"Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa mbalimbali za kitaifa na kimataifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma," alisema Magufuli kupitia taarifa hiyo.

Dkt Augustine Mahiga akutana na mwanadiplomasia wa taifa lingine.
Dkt Augustine Mahiga akutana na mwanadiplomasia wa taifa lingine.

Mahiga, ambaye pia alihudumu kama Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo la Afrika Mashariki kutoka mwaka wa 2015 hadi 2019, awali alikuwa balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa kati ya mwaka wa 2003 na 2010.

Baada ya hapo alihudumu kama mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, akisimamia kitengo cha Siasa kati ya mwaka 2010 na 2013.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG