Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 30, 2024 Local time: 21:31

Wazimbabwe wasubiri kuapishwa rais mpya


Baadhi ya wananchi wa Zimbabwe wakiondosha picha ya Rais Robert Mugabe ukutani mara baada ya kujiuzulu.
Baadhi ya wananchi wa Zimbabwe wakiondosha picha ya Rais Robert Mugabe ukutani mara baada ya kujiuzulu.

Wananchi wa Zimbabwe wanasubiri kuapishwa kwa rais mpya kufuatia hatua ya Robert Mugabe kujiuzulu kutoka katika nafasi hiyo.

Mugabe ambaye amemaliza utawala wake uliodumu kwa miaka 37 atakumbukwa kwa utawala wa mabavu.

Marekani imepokea kitendo cha Mugabe kuondoka madarakani kwa kutoa wito kwa nchi hiyo kufanya uchaguzi uliyokuwa huru na haki.

Wakati huohuo mitaa ya Harare, mji mkuu wa Zimbabwe, ilikuwa imefurika watu waliokuwa wakisherekea kuondoka kwa kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari nchini Zimbabwe makundi ya watu walionekana wakishangilia katika mitaa ya Harare wakati habari zikienea kuwa Rais Robert Mugabe alikuwa amejiuzulu baada ya kutawala kwa miaka arubaini.

Spika wa Bunge la Zimbabwe Jacob Mudenda alisoma kile alichosema ni barua iliyokuwa imetoka kwa Rais Mugabe akitangaza rasmi kujiuzulu.

Wakati baadhi ya watu wanamchukulia Mugabe kuwa ni kiongozi ambaye alipigania uhuru wa Zimbabwe, watu wengine walikuwa na furaha kuona utawala wake unafikia kikomo.

“Sisi Wazimbabwe tunafuraha” na mtu mwengine alisema “ tunasherekea uhuru wetu.”Utawala wake, baadhi ya wachambuzi wanasema, uliiangamiza Zimbabwe.

“Ukiangalia nchi ambayo ilikuwa na uchumi imara, na kiwango bora kabisa cha elimu na mfumo wa afya, ni iliyokuwa na wasomi wa juu na wataalamu. Alichokifanya Mugabe kwa kujiuzulu kwa ajili ya uchumi, kwa dhana ya mapinduzi yaliyokubalika na wengi na kuzuilia demokrasia ni kitendo kiovu sana.
Wengine wamesema Mugabe angeweza kuepusha kufikia mwisho huu kama angeliamua kuachia madaraka mapema.

XS
SM
MD
LG