Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 06:54

Mahakama yaombwa kumpa Mladic kifungo cha maisha


Ratko Mladic akiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa The Hague
Ratko Mladic akiwa kwenye Mahakama ya Kimataifa The Hague

Majaji wa Umoja wa Mataifa huko the Hague wako tayari kutoa hukumu Jumatano katika kesi inayo mhusisha kiongozi wa zamani wa kijeshi wa Bosnian Serb Ratko Mladic.

Kiongozi huyo anatuhumiwa kwa makosa ya jinai ya kivita yaliyotokea wakati wa mgogoro wa iliyokuwa Yugoslavia katika miaka ya 90.

Mladic, anayejulikana kama “Chinjachinga wa Bosnia,” ni kiongozi wa mwisho wa kijeshi kukabiliwa na tuhuma za jinai katika mahakama hiyo maalum, iliyowekwa kushughulikia na mauji ya vita vya Bosnia vilivyoshamiri kutoka mwaka 1992 hadi 1995.

Mladic, ambaye amekuwa akikabiliwa na mashtaka hayo tangu 2012, ametuhumiwa na makosa ya mauaji ya halaiki 11, jinai za kivita dhidi ya ubindamu kwa madai ya kuhusika kwake kuongoza kampeni ya kuwaua kwa kuvizia kwa risasi watu huko Sarajevo na mauaji ya 1995 ya zaidi ya Waislam wanaume na wavulana 8,000 huko Srebrenica – mauaji mabaya kuliko yote yaliyowahi kutokea Ulaya tangu Vita vya Dunia II.

Waendesha mashtaka katika kesi wameitaka Mahakama ya Kimataifa The Hague (ICT) kumpa adhabu ya kifungo cha maisha Mladic.
###

XS
SM
MD
LG