Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 06:49

Wawakilishi wa Libya watangaza nafasi za kazi kujaza taasisi za kiutawala


Jan Kubis ametangazwa kuwa mwakilishi mpya maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya akichukua nafasi ya Stephanie Williams.
Jan Kubis ametangazwa kuwa mwakilishi mpya maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya akichukua nafasi ya Stephanie Williams.

Wawakilishi kutoka makundi hasimu nchini Libya wametangaza utaratibu wa watu kuwasilisha majina yao kwa ajili ya kujaza nafasi muhimu za taasisi za kiutawala kuanzia Jumanne.

Uamuzi huo umechukuliwa baada ya mazungumzo mapya yaliyo fanyika mwishioni mwa wiki nchini Morocco yanayo lenga kumaliza mgogoro uliodumu nchini humo kwa muda mrefu.

Utaratibu huo unaotarajiwa kumalizika Februari 2, 2021 ukiwa na lengo la kujaza nafasi kadhaa kwenye utawala wa mpito utakaobuniwa wiki ijayo mjini Geneva.

Mazungumzo hayo yaliyo anza Ijumaa kwenye mji wa Bouznika ulioko kusini mwa mji mkuu wa Rabat yaliwaleta pamoja wawakilishi kutoka kundi la Tobruk linalodhibiti eneo la mashariki ya Libya na wale kutoka baraza la utawala mjini Tripoli linaloshauri serikali ya GNA inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa.

Moussa Faraj ambaye ni mmoja wa waakilishi wa baraza linalo shauri serikali amesema kuwa mkutano huo ulitathmini mapendekezo ya nakala ya 15 ya makubaliano ya kisiasa ya Libya yaliotiwa saini mjini Skhirat hapo Decemba 17, 2015.

Faraj, Mwakilishi baraza la kiutawala la Libya anaeleza : "Baada ya mashauriano, tulikubaliana kuunda makundi madogo yatakayoongoza utaratibu wa kujaza nafasi kwenye utawala wa kitaifa. Kuna nafasi ya mkuu wa utawala pamoja na naibu wake, mhasibu mkuu pamoja na naibu wake, mkuu wa kupambana na rushwa na naibu wake pamoja na mkuu na wanachama wa tume ya uchaguzi ya Libya."

Taarifa ya pamoja iliyotolewa Jumapili inasema kwamba wajumbe kwenye mkutano huo pia walikubaliana kuunda makundi madogo ya kupanga mikakati ya mchakato wa kujaza nafasi hizo ambazo kwa muda mrefu zimekuwa kiini cha migogoro kati ya makundi hasimu ya kiutawala.

Mazunguzo hayo ndiyo ya mwisho miongoni mwa mengine yalioanza mwezi Septemba, 2020 katika taifa hilo la kifalme la Afrika Kaskazini

Wakati huo huo Jan Kubis ametangazwa kuwa mwakilishi mpya maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya Libya akichukua nafasi ya Stephanie Williams, uteuzi ambao umekaribishwa na Morocco kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Morocco Nasser Bourita.

Stephanie Williams
Stephanie Williams

Bourita ameeleza kuwa : "Jan Kubis ni mtaalamu mwenye ujuzi kwa kazi hiyo. Morocco inaunga mkono juhudi za UN kama mfadhili wa mazunguzo ingawa watu wa Libya ndio wenye uamuzi wa mwisho. Kazi ya UN ni kubuni mazingira na kurahisisha shughuli kufanyika.

Mazunguzo mbali mbali yamekuwa yakiendela Geneva, Morocco pamoja na Misri tangu makundi yote mawili yalipo kubaliana kusitisha mapigano Oktoba 2020 mjini Geneva, licha ya kwamba kiongozi wa kundi la mashariki mwa Libya Khalifa Haftar amekuwa akitishia kurejea kwenye mapigano.

Kwenye moja ya mazungumzo mapema wiki iliopita mjini Geneva wawakilishi kutoka Libya walikubaliana kuweka mikakati ya kuchagua utawala wa mpito utakaoshikilia serikali hadi uchaguzi ufanyike Decemba 24.

Na Kwenye mazunguzmo mengine ya Jumatano nchini Misri yaliofadhiliwa na UN, waliohudhuria walikubaliana kura ya maoni kuhusu katiba ya Libya ifanyike kabla ya uchaguzi wa Disemba.


XS
SM
MD
LG