Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 26, 2022 Local time: 15:07

Wajumbe kutoka pande hasimu Libya wakutana Morroco


Waziri Mkuu wa Libya anayetambulika kimataifa Fayez al Serraj akimkaribisha Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu kabla ya kuanza mkutano Tripoli, Libya Juni 17, 2020. Reuters.

Wajumbe kutoka utawala unaopingana nchini Libya wamekutana kwa mazungumzo yaliyofanyika Jumapili huko Morroco, zaidi ya wiki mbili baada ya pande hizo mbili kutangaza usitishaji mapigano.

Mkutano ulifanyika kutokana na juhudi za Morocco ambao walikuwa wenyeji wa mazungumzo ya amani mwaka 2015 ambayo yalipelekea kuundwa kwa serikali ya Libya iliyotambuliwa na umoja wa Mataifa, iliyoanza katika mji wa pwani ya Bouznika, kusini ya Rabat.

Mazungumzo yaliyopewa jina “mazungumzo ya Libya, yaliwajumuisha pamoja wanachama watano wa serikali ya kitaifa-GNA, yenye makao yake mjini Tripoli, na watano kutoka katika bunge lenye makao yake mashariki mwa Libya katika mji wa Tobruk.

Waziri wa mambo ya nje wa Morocco, Nasser Bourita katika matamshi yake kabla ya mkutano huo kuanza, alisema nchi yake inawapa Walibya “fursa” kujadili hoja ambazo zinazowagawa.

Ufalme upo tayari kuwapa Walibya fursa ya kujadili maswala kulingana na mapenzi yao, na itawapongeza bila kujali matokeo, Bourita alisema.

Morocco haina ajenda au mpango wa kuwasilisha kwa pande hizo mbili, aliongeza kusema hivyo Bourita.

Suluhisho la mzozo wa Libya lazima liamuliwe na walibya wenyewe, chini ya udhamini wa UN, alisema, kabla ya wajumbe kukutana kwa faragha.

Libya imepitia takribani muongo mmoja wa machafuko ya ghasia tangu ghasia zilizoungwa mkono na NATO mwaka 2011 zilizouangusha mna kumuua diktekta mkongwe Moamar Gadafi.

Wafuasi wa Khalifa Haftar wakiandamana mjini Tripoli.
Wafuasi wa Khalifa Haftar wakiandamana mjini Tripoli.

Mgogoro huo ulizidi kuwa mbaya mwaka jana wakati mwanajeshi mwenye nguvu, Khalifa Haftar, ambaye pia analiunga mkono bunge la Tobruk na anaungwa mkono na Misri, UAE Pamoja na Urusi alipoanzisha shambulizi la kuuteka mji mkuu Tripoli.

Haftar alipigwa tena mapema mwaka hu una vikosi vya GNA vinavyoungwa mono na Uturuki na mapigano sasa yamekwama kuzunguka mji wa Sirte huko Mediterranean, kwenye lango la kuelekea viwanda vya Mafuta huko mashariki mwa Libya na vituo vya kusafirisha nje bidhaa hizo.

Agosti 22, tawala zinazopingana zilitangaza kando kuwa zitasitisha uhasama wote na kufanya uchaguzi wa nchi nzima, na kupata sifa kutoka mataifa yenye nguvu Duniani.

Katika mkutano wa kilele wa januari mjini Berlin, nchi kuu zilizohusika katika mzozo wa Libya zilikubaliana kuheshimu zuio la silaha na kuacha kuingilia masuala ya ndani ya Libya.

Lakini Jumatano, mjumbe wa muda wa UN kwa Libya, Stephane Williams alishutumu kile alichokiita, “wasi wasi” na ukuikaji unaoendelea wa vikwazo vya silaha katika nchi hiyo iliyopo Afrika kaskazini. Kulingana na ripoti kutoka kwa wataalamu wa UN, vikwazo vya silaha bado havina tija kabisa na ukiukaji ni mkubwa ulio wazi.

Waandamanaji wakusanyika kupinga serikali Tripoli, Libya, August 25, 2020. REUTERS/Hazem Ahmed NO RESALES. NO ARCHIVES
Waandamanaji wakusanyika kupinga serikali Tripoli, Libya, August 25, 2020. REUTERS/Hazem Ahmed NO RESALES. NO ARCHIVES

Williams alisema Ujumbe wa Umoja wa Mataifa-UNSMIL pia ulikuwa ukipokea ripoti za uwepo mkubwa wa mamluki na wafanyakazi wa kigeni nchini Libya, na kuongeza kuwa hii inaleta mkanganyiko katika nafasi za makazi ya baadae.

Mkutano wa Jumapili huko Morocco uliambatana na mazungumzo huko Instanbul, kati ya Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan na mkuu wa GNA, Fayez al Sarraj, rais wa Uturuki alisema bila kufafanua.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG