Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 14:47

Mazungumzo ya amani ya Libya yasitishwa Moscow


Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nchi za nje wa Rashia, Uturuki na Rashia wakijadili suala la Libya Moscow.
Mawaziri wa ulinzi na mambo ya nchi za nje wa Rashia, Uturuki na Rashia wakijadili suala la Libya Moscow.

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Rashia Sergey Lavarov, anasema kwamba mazungumzo ya kusitisha mapigano nchini Libya yameendelea vizuri Jumatatu kukiwa na matumaini ya kufikiwa makubaliano.

Akizungumza mjini Moscow Jumanne baada ya kukutana na waziri mwenzake wa Sri Lanka, Lavarov anasema kiongozi wa Jeshi la Kitaifa la Libya, LNA, Jenerali Khalifa Haftar ameomba siku mbili zaidi ili kuweza kujadili na washirika wake juu ya mkataba wa kusitisha mapigano ulopendekezwa na Uturuki na Rashia.

Waziri mkuu wa serikali ya Libya inayotambuliwa na Umoja wa Mataifa Fayez al-Serraj alitia saini mkataba huo siku ya Jumatatu, unaotaka usitishaji mapigano bila ya masharti yeyote.

Wakati huo huo mjini Ankara, rais Tayyip Erdogan wa Uturuki amemonya Jenerali Hafter kwamba atampa funzo kali akijaribu kuanza tena vita baada ya kuondoka Moscow bila ya kutia saini mkataba wa kusitisha mapigano.

"Hatuta sita kutoa funzo linalostahiki dhidi ya kiongozi aliyeasi Hafter akiendeelea na mashambulio yake dhidi ya utawala uanotambuliwa wan chi hiyo na ndugu zetu wa Libya." amesema rais Erdogan

Akiuhutubia mkutano wa chama chake mjini Ankara Jumatatu, Erdogan anasema mazungumzo ya Moscow yameendelea vizuri mjini Moscow na kwamba suala hilo litajadiliwa zaidi wakati wa mkutano wa Berlin siku ya Jumapili. Mkutano huo utahudhuriwa na mataifa ya Ulaya, Afrika Kaskazini, Mashariki ya Kati pamoja na Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika na Umoja wa nchi za Kiarabu.

XS
SM
MD
LG